Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Msemaji wa manispaa ya Rotterdam aliliambia shirika kubwa zaidi la habari la Uholanzi kwamba maandamano hayo yalifanyika katika mazingira mazuri na ya amani. Maelfu ya watu, wakiwemo familia nyingi pamoja na watoto wao, walishiriki katika maandamano hayo ambayo yalipitia njia ya kutokea msikiti wa Al-Salaam huko Rotterdam hadi ukumbi mkubwa wa jiji katikati ya mji huo. Waandamanaji walikuwa wamebeba bendera za Palestina na mabango yenye maandiko ya kulaani vita na mauaji ya Wapalestina.
Katika mahojiano na moja ya mashirika ya habari ya Rotterdam, "Bwana Azedin Karat" alielezea ushiriki mkubwa wa wananchi kuwa ni ujumbe wa wazi kwa serikali ya Uholanzi, akieleza matumaini yake kuwa, jambo hilo litasababisha kuchukuliwa kwa hatua zaidi za kuzuia mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel.
Maoni yako